Monday, January 16, 2012

Prezzo Peter Kenneth

Vijana yenyewe tumesuffer ya kutosha jo. Cheki hii story, hakuna mtu hutujali kwa hii gava. Vile walifanya tu ni ku create ministry ya ma youth eti tucheki kama wanatumind but hawatufikirii kabisa. Ma vijana sisi ni wengi na kuna vile tunaweza leta change kwa motherland tukishikana poa. Vijana shinda zao across Kenya ni the sama. Tia zii ukabila. Ukicheki kila place vile jo vijana wamekosa ma job hata wakiwa na masomo. I say GOK yenyewe imetu marginalize sana. Checki wasee most ambao wamezaliwa after 1973 uone hatuna life. Masomo mapero walitupatia but serikali ikafuck system. Ukiona kijana akiamua kutoka mtaani anaenda mpaka ku join Alshabab yenyewe kusema ukweli ni sababu ya msoto. By the end of the day lazima watu wakule na wavae. Sasa hii gava imetufinya mpaka the most basic stuff ni noma kuata. Population vile iliongezeka ma leaders hata unashindwa walikuwa wanafanya nini. Sisi kama vijana lazima sasa tushikane na tusimame kindete pamoja. Tunataka prezzo na leadership ya power. Haitakuwa job rahisi vile but atleast tunataka wasee wakiingia kwa mbunge wanajaribu. Mimi nacheki hii race ya ma election naona kuna noma sababu kila mtu sasa anatafuta kura tuu. Ukicheki msee kama Rao sasa, amekuwa kwa hiyo hao tangu lini? Yeye kama mp wa Kibich ni nini amefanyia mavijana? Sasa itakuwa aje tutrust msee mpaka akiwa hapo sijawahi sikia akitetea ma youth jo. Kuna vile hiyo ni blunder noma sana. Cheki sasa UK, huyu ni kijanaa ndio but amefanya nini pia? Vile sasa nasikia amerankiwa na ndoo ni nini amefanyia the marginalised youth? Mimi na checki siasa za UK na Rao kuna vile ni extension ya wale watu wamekuwa wakitufinya tangu uhuru. Tena kwani kenya ni Dynasty eti vile ma pero wao wali lead ma grandapa na mapero wetu tena watoi wao watuongoze. Hapo ni zii, hata akina mama zetu wamezaa ndume pia. Niwakati wa new comer sasa kuchukuwa uongozi. Cheki PK wetu sasa. Naona huyu msee hata akibonga kuna vile anaamini vile anasema. Hapayuki sana na sijamusikia akipatiana vitendawili na hajashikwa na typo til sasa. Mimi kama kijana naona PK kama ni msee kila kijana Kenya anaweza trust. Yenyewe jo lazima tufanye kitu. Najuwa siasa saa hii kuna vile ni za ukabila but hiyo itatuumiza sisi kama vijana. Pk akapiga collabo na Tuju inaweza kuwa poa sana. Then hata akina Keiyapi tuwaingize hapo. Na checki itakuwa poa kusukuma hawa wanasiasa wazee nje  sasa coz hata hawatuelewi sasa. Cheki vile dunia imechange na tech zimecome then tunapeleka ma grey hair kutuwakilisha. Ma vijana tugutuke na tupige Darubini vipoa, hii ni story ya life wetu jo. Vijana na pk tulete maendeleo kwa hii nchi. Mungu abariki Kenya.